Watuhumiwa wa escrow wabanwa mbavu Zanzibar

tibaijukaZanzibar. Taasisi za kutetea haki za binadamu na kusimamia misingi ya Utawala Bora Zanzibar zimesema viongozi waliohusishwa na ufisadi wa Sh 306 bilioni kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow wakamatwe na kufikishwa mahakamni badala ya kufukuzwa kazi peke.

Msimamo huo umetolewa na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) na Taasisi ya Utafiti na Sera za Kijamii Zanzibar (ZIRPP) baada ya waliotajwa katika sakata la escrow kung’oka na mmoja kusimamishwa kazi.

Rais wa ZLS, Awadhi Ali Said alisema viongozi waliohusika haitoshi kujiuzulu bila ya kufunguliwa mashtaka kwa vile kuna makosa ya jinai yamefanyika katika kashfa hiyo.

Alisema viongozi walioonyesha udhaifu wa kiutendaji na uzembe hadi kusababisha fedha hizo kuiibiwa wanapaswa kujiuzulu kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamojahata kama hawakuhusika moja kwa moja katika uchotaji wa fedha hizo.

Hata hivyo, alisema kazi ya kupambana na rushwa na ufisadi itaendelea kuwa ngumu kama jamii itaendelea na tabia ya kuwapokea kama mashujaa viongozi wanaofukuzwa katika nyadhifa zao kutokana na kuhusishwa na kashfa za ufisadi.

Pia, alisema kwamba ZLS inaamini kuwa katika uwajibikaji wa pamoja Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatakiwa kujiuzulu.

Mkurugenzi Mtendaji wa (ZIRPP) Muhammed Yussuf Mshamba alisema kulingana Ripoti ya CAG, Gavana wa Benki Kuu na Waziri wa Fedha wanapaswa kujiuzulu ili kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamoja.

“Tukisimama katika misingi ya uwajibikaji wa pamoja Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Gavana wa BOT na Waziri wa Fedha waondoke kulinda heshima zao na kupunguza machungu ya wananchi,” alisema Mshamba. Alisema fedha zilizopotea ni fedha za umma kwa sababu Tanesco ndiyo walikuwa wakikusanya tozo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

One Reply to “Watuhumiwa wa escrow wabanwa mbavu Zanzibar”

  1. Hakika wakamatwe, walazimishwe kurejesha fedha zote, popote walipozipeleka kwa kuanza na kutaifishwa malizao za wizi na hatimae wende jela kwa kosa lao la wizi na ujambazi uliofanyika kwa njia yeyote ile ikiwa ni ya hadaa au ya nguvu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s