Balozi Iddi: Masheha msiogope kutekeleza majukumu yenu

Balozi Seif Ali Idd akizungumza na wana Polisi Jamii na wananchi wa Jimbo la Chambani mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la jengo la Ofisi yao hapo katika Kijiji cha Chambani. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Mwanajuma Majid.
Balozi Seif Ali Idd akizungumza na wana Polisi Jamii na wananchi wa Jimbo la Chambani mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la jengo la Ofisi yao hapo katika Kijiji cha Chambani. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Mwanajuma Majid.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema Masheha na Wakuu wa Wilaya hawapaswi kutishika wanapotekeleza majukumu yao waliyokabidhiwa na Serikali hususani suala la uandikishaji wa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.

Alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha mtu asiye na sifa ya kujiandikisha kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho hivyo hastahiki kupewa ili kuiepusha Serikali kupata hasara ya kutengeneza vitambulisho ambavyo baadaye vinaharibika bila ya kuchukuliwa na wale waliojiandikisha.

Balozi Iddi alitoa kauli hiyo baada ya kuweka jiwe la msingi la Maskani ya CCM ya Tuheshimiane yenye wanachama  105 waliohama Chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM katika Kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Balozi Seif alisema wapo vijana wengi waliojiandikisha kwenye vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi hasa katika Kisiwa cha Pemba wakitokea maeneo ya Tanga, Tanzania Bara na Mombasa, nchini Kenya wakielewa kwamba kitendo chao ni kosa la jinai na ndizo sababu zilizopelekea kushindwa kuchukua vitambulisho hivyo baada ya kutengenezwa na hatimaye kuitia hasara Serikali.

Alionya kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi pamoja na taasisi zinazohusika itahakikisha kuwa mtu asiye na sifa kamwe hatapata fursa hiyo na wale watakaoamua kufanya ujanja haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika hao.

Balozi Seif aliwapongeza Vijana hao wa Makangale kwa uamuzi wao wa kuacha kuunga mkono vyama vya upinzani na kujiunga na CCM chenye sera zinazotekelezeka sambamba na kuthamini watu wote bila ya ubaguzi.

Chanzo: Nipashe
Advertisements

One Reply to “Balozi Iddi: Masheha msiogope kutekeleza majukumu yenu”

  1. kwanza tunataka tumwambie huyo kiumbe kuwa yeye hana asili ya Zanzibar 100%. pili hivo vipande vya makaazi ,anavyovizungumzia Tukiwa sisi Wazanzibari wazaliwa atatuambiaje tuwe wakaazi na hali sisi ni wananchi, mkaazi ni yeye asiekua na asili ya Kizanzibari vitambulisho hivi mwisho wake 2015 ishatha. NA nyie Masheha ikiwa kwenu ni Zanzibar basi msichezewe na vipita njia kama hoyo Jitu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s