Mawakili wakwamisha kesi ya Ponda kusikilizwa

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto) akizungumza jambo na mawakili wake, Juma Nasssoro   baada ya kuahirishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro. Picha na Juma Mtanda
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto) akizungumza jambo na mawakili wake, Juma Nasssoro baada ya kuahirishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro. Picha na Juma Mtanda

Morogoro. Kesi inayomkabili katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekh Ponda Issa Ponda jana ilishindikana kusikilizwa, huku mawakili wa pande mbili za mashtaka na utetezi wakivutana kuhusu haki ya mshtakiwa kupewa dhamana.

Kesi hiyo, iliyo mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, Mary Moyo, ilitajwa jana na kulizuka mabishano kuhusu kuanza rasmi kusikilizwa pamoja na mtuhumiwa kupewa dhamana.

Akiwasilisha hoja ya upande wa utetezi, wakili kiongozi Juma Nassoro aliwasilisha maombi matatu kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Katika ombi lake la kwanza, alitaka kesi hiyo ianze kusikilizwa kwa sababu taratibu zote za awali kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, zimekamilika.

Wakili huyo alisema kama kuna nyongeza au mabadiliko kwa upande wa mashtaka, yanaweza kufanyika huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa. Ombi lake la pili, alitaka Mahakama kulifuta shtaka la kukiuka amri ya Hakimu Mkazi wa Kisutu iliyotolewa Mei 9, 2013 ambayo ilitoa adhabu ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kumtaka mshtakiwa asifanye jambo lolote la uvunjifu wa amani na badala yake ahubiri suala la amani.

Wakili huyo aliiambia mahakama, mshtakiwa alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga hukumu hiyo, na katika hukumu iliyotolewa Novemba 27, mwaka huu na Jaji Augustine Shangwa alifuta hukumu ya Mahakama ya Kisutu ambayo ndiyo msingi wa shtaka namba moja la kesi iliyopo katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.

Wakili huyo mtetezi alisema kutokana na hukumu iliyotolewa na Jaji Shangwa, shtaka namba moja halina uhalali, hivyo mahakama inapaswa kuliondoa au kutoa mwongozo.

Katika ombi lake la tatu, wakili huyo aliomba Mahakama kutoa dhamana kwa mshtakiwa kwa kuzingatia hukumu ya Jaji Shangwa.Wakili mwingine wa mshtakiwa, Bathoromew Tarimo alisisitiza kuwa kutokana na hukumu hiyo hati ya mashtaka imebomoka pamoja na hati ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DDP).

Hata hivyo, upande wa mashtaka ulipinga maombi hayo matatu.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s