Maalim Seif aitabiria CUF ushindi mkubwa

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wanachama na wananchi wa jimbo la Magogoni wakati alipofanya ziara ya kufungua ofisi za chama na kuzindua miradi ya maendeleo

Zanzibar. Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema upepo wa kisiasa unakivumia vizuri chama chake na ana matumaini Uchaguzi Mkuu ujao kitapata viti 18 vya uwakilishi katika ngome ya CCM Unguja.

Hivi sasa CUF inashikilia majimbo manne ya Unguja kati ya 32 na kwa muda wote ngome yake imekuwa ni Pemba kinakoshikilia majimbo yote 18.

Akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Magogoni, Wilaya ya Magharibi Unguja, Maalim Seif alisema suala la Katiba Mpya na ufisadi uliokithiri vitaipa wakati mgumu CCM, hasa upande wa Zanzibar.

“Hivi sasa Unguja tuna majimbo manne, lakini katika uchaguzi mkuu ujao tutapata si chini ya 18 ukijumuisha na 18 ya Pemba, CUF tutaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa tukiwa na nguvu ya uamuzi,” alisema Maalim Seif.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wanachama na wananchi wa jimbo la Magogoni wakati alipofanya ziara ya kufungua ofisi za chama na kuzindua miradi ya maendeleo
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wanachama na wananchi wa jimbo la Magogoni wakati alipofanya ziara ya kufungua ofisi za chama na kuzindua miradi ya maendeleo

Maalim Seif alisema CUF inaweza kupata majimbo zaidi ya hayo Unguja, lakini dhamira yake ni kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hivyo si busara viti vyote vya uwakilishi na ubunge vikawa vinashikiliwa na chama hicho.

Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kutokana na maridhiano yaliyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), alisema CCM wanajua hali ni mbaya upande wa Zanzibar na hivi sasa baadhi ya viongozi wake wamekuwa wakisikika wakisema, “hatutoi Serikali”.

“Silaha yetu ni mshikamano wetu tukishikamana, hakuna wa kutuzuia kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wanaoamua ni wananchi si Maalim Seif, si Shein wala si Balozi Seif Ali Iddi,” alisema Maalim Seif.

Alisema hakuna Mzanzibari aliye tayari kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa kwa sababu inainyonga Zanzibar, hivyo ni wazi suala hilo lina ufisadi.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiwasalimia viongozi wa Polisi Jamii Shehia ya Kinuni, jimbo la Magogoni; Kulia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Mhe. Abdillahi Jihad Hassan.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiwasalimia viongozi wa Polisi Jamii Shehia ya Kinuni, jimbo la Magogoni.

Kuhusu ongezeko la matukio ya uhalifu, alisema yatadhibitiwa kwa jamii kuunga mkono dhana ya ulinzi shirikishi.

Alisema Jeshi la Polisi peke yake haliwezi kumaliza matukio ya uhalifu, ikiwamo ujambazi, watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya na watu wanaofanya udhalilishaji watoto na wanawake, lakini jamii kupitia mpango wa ulinzi shirikishi ndio watakaoyamaliza.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s