Kikwete achochea mjadala Escrow

Sehemu ya wazee wa Mkoa Dar es Salaam wakishangilia kuunga mkono kufukuzwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana.
Sehemu ya wazee wa Mkoa Dar es Salaam wakishangilia kuunga mkono kufukuzwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana.

Dar/mikoani. Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow imepokewa kwa hisia tofauti na wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida, wengi wakionyesha kutoridhishwa na hatua alizochukua.

Akizungumza kwa simu baada ya hotuba hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kitendo chake cha kuwatetea waliohusika katika kashfa hiyo ya uchotwaji wa Sh306 bilioni kitakigharimu chama chake cha CCM siku chache zijazo.

Alisema kuachwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi si cha kupongezwa kwa sababu viongozi hao ndiyo wahusika wakuu wa kashfa hiyo.

“Ameonyesha kuwa kazi iliyofanywa na Bunge, ikiwahusisha mawaziri aliowateua waliotumia uchunguzi uliofanywa na vyombo vya Serikali ni bure kabisa. Hotuba yake ina maana kuwa uchunguzi wa Ikulu ndiyo unaotakiwa kuaminika.”

Huku akionyesha kukerwa na jinsi Rais Kikwete alivyokuwa akiyarudiarudia maazimio ya Bunge, Mbowe alisema katika hotuba yake, Rais Kikwete amekiri kuwa miamala yote ya fedha iliyofanyika katika benki ilikuwa halali, kitu ambacho si kweli.

“Profesa Tibaijuka ametolewa kafara tu. Huyu alikuwa katika tawi tu la kashfa ya escrow, wahusika wakuu walikuwa ni Muhongo na Maswi ila wameachwa. Rais anatetea watu badala ya kuwachukulia hatua. Hakika anazidi kuchochea moto,” alisema.

Aliongeza, “Tunaitakia CCM maisha marefu na Rais Kikwete ili siku moja waje waone jinsi kauli ya Rais kuhusu escrow itakavyoitafuna CCM. Inakuwaje Rais anashindwa kusoma hisia za Taifa juu ya jambo hili?”

Wakati Mbowe akieleza hayo, wasomi mbalimbali nchini wamepongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Kikwete huku wakiwashauri viongozi waliotajwa katika maazimio ya Bunge kwamba mamlaka za uteuzi ziwawajibishe, wajiuzulu wenyewe kabla ya majibu ya uchunguzi dhidi yao hayajatoka.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kauli, hotuba na hatua za Rais Kikwete ni kuwapaka Watanzania mafuta kwa mgongo wa chupa.

“Kimaadili, viongozi wote waliotajwa kuhusika kwenye sakata la escrow walipaswa kujiuzulu. Rais alistahili kuwaagiza waachie ngazi na wasipofanya hivyo, awawajibishe. Siyo kupaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa kama alivyofanya kwenye hotuba yake.”

Alisema Taifa liko katika hali tete, huku wahisani wakisimamisha misaada ya kimaendeleo, lakini Rais haonekani kuchukua hatua madhubuti siyo tu kurejesha imani ya wananchi na wahisani kwa Serikali, bali kunusuru nchi.”

Zitto awaachia wananchi

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s