Polisi mmoja afariki wanne wanusurika mmoja apotea

FUKWE YA BAHARI
                                        Fukwe ya bahari maeneo ya Kaskazini Unguja

Polisi mmoja amefariki dunia na wenzake wanne wameokolewa baada ya boti yao waliokuwa wakitumia katika doria ya jeshi la polisi kuzama katika eneo la Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja, Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Juma Saad Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana usiku ambapo alisema mtu mmoja bado hajapatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea. alisema tukio hilo limetokea majira ya saa saba usiku baada ya mashine ya boti hiyo kupata khitilafu na boti kupigwa na dhuruba ya upepo mkali na kusababisha boti kubiruka na kuzama. Kamanda Khamis amemtaja aliyefariki ni Said Hassan Saleh ambaye ni miongoni mwa wazamiaji wazuri kutoka idara ya polisi.

Waliookolewa katika tukio hilo wametajwa kuwa ni Koplo Mbaraka Nambari zake ni E837, Mahmoud Nambari zake ni J1320 PC. Haji Khamis Namba zake ni F4578 pC, na Farid Mohammed Suleiman ambaye Namba zake ni K1627 PO.

Hata hivyo Kamanda Khamis amesema polisi hao bado wapo hospitali ya Mnazi Mmoja na wanaendelea vizuri.

Aidha alisema jumla ya polisi sita waliokuwemo katika boti hiyo ambayo iikuwa katika kazi zake za doria ya kawaida lakini mtu mmoja bado hajaonekana lakini jeshi hilo linaendelea na juhudi na kumtafuta.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s