Tumejipanga kuiangusha CCM Z’bar- CUF

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Zanzibar Ismail Jussa Ladhu
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Zanzibar Ismail Jussa Ladhu

Zanzibar. Chama cha Wananchi CUF Zanzibar kimesema kwamba kimejipanga vizuri kwa Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba mwaka 2015 kuliko chaguzi zote zilizofanyika visiwani Zanzibar tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ili kuhakikisha inaing’oa CCM madarakani.

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa baraza kuu la chama hicho, Ismail Jussa Ladhu alipohutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shamiani, Chake Chake Kisiwani Pemba juzi, ambapo pia alidai kuwa watu 12,000 walinyimwa haki ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 jambo lililoathiri matokeo ya uchaguzi huo.

“Uchaguzi wa mwakani, CCM tunawalaza chini kwa sababu hatujawahi kujipanga kwa uchaguzi kama mwaka huu,” alisema Jussa.

Alisema kwamba pamoja na CCM kuendelea kufanya kampeni za chinichini katika ngome ya CUF kisiwani Pemba, haitafanikiwa kupata jimbo hata moja kati ya 18 yaliyopo kisiwani humo.

Kuhusu watu waliokosa haki ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, Jussa alisema walinyimwa fursa ya kujiandikisha na kupiga kura kwa sababu za kisiasa ikiwa ni mbinu ya kuibeba CCM na kwamba kitendo hicho ni kinyume na haki za binadamu.

Katika uchaguzi huo Mgombea wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein aliibuka na ushindi wa asilimia 51 dhidi ya mgombea wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, aliyepata asilimia 49.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s