‘Wanaume mnaopigwa na wake zenu jitokezeni’

Kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni woga, aibu na kasumba ya mfumo dume, wanaume wanaonyanyaswa wamekuwa wakificha aibu hiyo na kuendelea kubaki katika unyanyasaji huo.
Kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni woga, aibu na kasumba ya mfumo dume, wanaume wanaonyanyaswa wamekuwa wakificha aibu hiyo na kuendelea kubaki katika unyanyasaji huo.

Ni nadra kusikia mwanamume akilalamika kuwa amepigwa na mke au mwenza wake. Suala hilo ni adimu zaidi katika nchi za Afrika hasa zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zimefunikwa na blanketi la mfumo dume. Kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni woga, aibu na kasumba ya mfumo dume, wanaume wanaonyanyaswa wamekuwa wakificha aibu hiyo na kuendelea kubaki katika unyanyasaji huo.

Kutokana na ongezeko la matukio ya wanaume kunyanyaswa na wake au wenza, Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, (Tawla) kimetoa wito kwa wanaume kujitokeza ili kupata msaada wa kisheria pindi wanaponyanyaswa.

Mwenyekiti wa asasi zisizo za kiserikali za katiba na jinsia, (Zec) zinazoratibiwa na Tawla, Victoria Mandari anasema matukio hayo ni mengi lakini wanaume wamekuwa wakiyafanya kuwa siri pengine kwa kuona aibu.

“Wanaume watafute chama kitakachowasaidia kutetea haki zao na kutengeneza hata sheria ambazo zitawasaidia kupata haki zao,” anasema. Anasema sheria zinasema kuwa asiwepo mwanandoa anayemnyanyasa mwenzake kijinsia, hivyo basi hata wanaume nao hawatakiwi kunyanyaswa.

“Tatizo ni kuwa wanaume hawajitokezi wanaponyanyaswa, waseme ili wasaidiwe,” anasema.

Matukio ya wanaume kunyanyaswa na wake zao yameendelea kutokea huku wanaume wakidai kuwa unyanyasaji huo unachochewa na wingi wa vyama, asasi, na mashirika yanayotetea haki za wanawake pekee.

Mwaka jana, Naibu Kamishna wa Polisi, Adolphina Chialo alisema wanaume wengi sasa wanakwenda kushtaki katika madawati ya kijinsia ya polisi pale wanaponyanyaswa.

Inaelezwa kuwa hata wanawake wanaowanyima unyumba waume zao bila sababu maalumu nao wanafanya unyanyasaji wa kijinsia.

Kamishna Chialo anasema wapo wanaume wanaofika vituo vya polisi wakiwa na majeraha baada ya kupigwa na wake zao.

Katiba Inayopendekezwa

Pamoja na unyanyasaji kwa wanaume, wanasheria hao walizungumzia Katiba Inayopendekezwa na kusema kuwa licha ya kupingwa na taasisi nyingi za kijinsia na kisheria nchini, kwa upande wao imezingatia masuala ya jinsia ambayo awali, hayakutambuliwa katika Katiba ya sasa.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s