SUK isibezwe, imeleta utulivu na amani Zanzibar

dksheinmaalimseif

Tunashangazwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa CCM huko Zanzibar kwamba wanachama wa chama hicho wamechoshwa na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Mmoja wa viongozi hao ni Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, Salmin Awadh Salmin (CCM), ambaye ameendeleza kampeni ya kuwataka Wazanzibari kuikataa SUK, akisema muundo wa serikali hiyo hauna faida wala masilahi kwa Zanzibar.

Akihutubia mkutano wa chama hicho katika Jimbo la Mwanakwerekwe hivi karibuni akiwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa SMZ, Shamsi Vuai Nahodha, ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo hilo, aliwataka viongozi wakuu wa chama hicho wasiwe na kigugumizi katika kuikataa SUK na akisema yeye na baadhi ya wawakilishi wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi kuikataa serikali hiyo.

Itakumbukwa kwamba Mei, mwaka huu mwakilishi huyo alihutubia mkutano wa CCM ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana mjini Zanzibar na kusema wawakilishi wenzake wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kwamba lengo na matumaini ya kuundwa kwa SUK yamefutika. Alisema ni vyema wananchi wakaulizwa kama bado wanahitaji mfumo huo au ule wa zamani urejeshwe.

Katika hali ya kushangaza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alimuunga mkono na kusema ni jambo muhimu kuitishwa kura ya maoni ili wananchi wapate nafasi ya kuulizwa kama wanataka mfumo wa Serikali iliyopo kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka ujao. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alimshambulia Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kudai kwamba amekuwa na “tabia ya kubadilisha ajenda za kisiasa na kutikisa misingi ya umoja wa kitaifa nchini”.

Sisi tunadhani wanasiasa wanaohoji au kupinga kuwapo kwa SUK wamesahau Zanzibar ilikotoka, hivyo hawastahili kuwa viongozi. Tunasema hivyo kwa kuwa viongozi hao wanakwenda kinyume na uamuzi wa vyama vyao ambao ulipitishwa na kuridhiwa na vikao vyote vya juu, kabla muundo wa SUK haujapitishwa na wananchi wa Zanzibar kupitia kura ya maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Tumekuwa tukisema mara kwa mara kwamba sisi ni waumini wakubwa wa Muungano ambao SUK ni sehemu yake. Kwa maneno mengine, tunasema kuiyumbisha SUK ni kuuyumbisha Muungano na kuuyumbisha Muungano vilevile ni kuiyumbisha SUK. Katika hali hiyo, tutakuwa hatutimizi wajibu wetu iwapo tutakaa kimya pale tunapoona kuna hatari inayoweza kusababisha nyufa katika msingi wa Muungano wetu.

Tungependa kuwashauri tena viongozi wa CCM na CUF kuilinda SUK kama mboni za macho yao. Wasisahau kwamba SUK ilitokana na maridhiano baina ya vyama hivyo baada ya kuwapo machafuko ya muda mrefu kutokana na siasa za visasi na utengano visiwani humo. Kutokana na ushindani mkubwa wa kisiasa uliopo kati ya vyama hivyo, amani itakuwapo iwapo vitashirikiana katika kuunda serikali ya pamoja kama ilivyo sasa.

Rai yetu kwa viongozi wa CUF na CCM ni kwamba tofauti kati yao hazitamalizika kwa kuivunja SUK, bali kwa mazungumzo na maridhiano. Wasikubali itikadi za vyama vyao ziwatenganishe, kwani wakati vyama hivyo vinaweza kufa, Zanzibar itaendelea kuwapo. Watafanya vyema iwapo watatambua kuwa, kuivunja SUK kutawakwaza wananchi na kuirejesha Zanzibar katika machafuko na zama za giza za ‘jino kwa jino’.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

2 Replies to “SUK isibezwe, imeleta utulivu na amani Zanzibar”

    1. Abuu Ali
      Kama alivyosema alietangulia hapo juu, walio na mawazo hayo wanahitaji kuchunguuzwa Uzanzibari wao. Lakini haishangazi kuona hivyo kwani kila inapoonekana dalili ya kupatikana faida na amani ya nchi ya Zanzibar na watu wake, jamaa huyu anaikandia. Lakini si shangai hata kidogo kwani huko kwao Yemen amani haiko na anafanya kazi ya umamluki kuikoroga Zanzibar. Ole wenu munaemuona wa maana. Kajificha ndani ya CCM kwa lengo lake huyu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s