Wekeni mikakati kukabili mabadiliko ya tabia nchi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, mh. Maalim Seif Sharif Hamad akifungua mkutano wa sita wa nchi za visiwa vidogo vya bahari ya Hindi huko Kilimani mjini Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, mh. Maalim Seif Sharif Hamad akifungua mkutano wa sita wa nchi za visiwa vidogo vya bahari ya Hindi huko Kilimani mjini Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesifu mkakati ulioanzishwa na nchi za visiwa vidogo katika Bahari ya Hindi kukabilina na athari za mabadiliko ya tabia nchi na majanga ya kimaumbile katika nchi zao.
Amesema hayo leo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa sita wa nchi za visiwa vidogo katika Bahari ya Hindi ISLANDS unaojumuisha nchi za Comoro, Madagascar, Mauritius, Seychelles na Zanzibar unaofanyika hoteli ya Zanzibar Ocean View, Kilimani mjini Zanzibar.

Amesema nchi za visiwa vidogo kama Zanzibar zinapaswa kuwa na mikakati imara inayoeleweka kujikinga na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na majanga ya kimaumbile mara yanapotokea.

Makamau wa Kwanza wa Rais amesema nchi hizo tayari zimeshuhudia athari mbaya kwa maisha ya watu, vitegauchumi na upotevu wa maliasili kutokana na matokeo ya majanga ya kimaumbile na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya uharibifu wa mazingira.

Maalim Seif amesema katika kujitayarisha na mkakati huo nchi hizo hazina budi kuwa na mashirikiano ya karibu na Jumuiya pamoja na Mashirika ya Kimataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kuziunga mkono nchi hizo kwa misaada ya kitaalamu na fedha.

“Lazima tuwe na mikakati ya pamoja iliyoandaliwa mapema kwa ajili ya kufuatilia na kujikinga na athari na majanga ya kimaumbile yanapotokea, ikiwemo kuwapa taaluma wananchi katika nchi zetu”, amesema Maalim Seif.

Amelipongeza shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Mkakati ya kupunguza majanga (UNISDR), Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia kwa mashirikiano makubwa inayozipa nchi hizo za visiwa katika kukabiliana na athari za kimazingira na majanga.

Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabilina na Majanga (UNSIDR), Kasuko Ishigaki amesema shirika hilo litaendeleza ushirikiano na nchi za visiwa vidogo katika Bahari ya Hindi katika kuzuia athari mbaya kwa maisha ya binaadamu na viumbe wengine.

Amesema hatua hizo zitahusisha kuziwezesha nchi za visiwa vidogo kuwa mipango madhubuti ya uhifadhi wa mazingira na kuepuka athari za mabadiliko ya tabianchi na kuona zinaingizwa katika mipango ya maendeleo ngazi za kitaifa.

Chanzo: OMKR

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s