Ahadi waliyofungamana viumbe na Allaah Kabla ya kuzaliwa kwao

Supplicating_Pilgrim_at_Masjid_Al_Haram._Mecca,_Saudi_ArabiaAllaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Alikusanya roho za binaadamu wote kabla ya kuumbwa kwao, zikafungamana ahadi Naye ya kukiri kwamba Yeye Ndiye Mola wao na kwamba watampwekesha bila ya kumshirikisha na zika ahidi pia kumtii

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ﴿١٧٢﴾أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ

Na (taja) pale Mola wako Alipowaleta katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao, na Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, (Akawuliza): “Je, Mimi siye Mola wenu?” (Wakajibu kwa) kusema: “Ndiye, tunashuhudia!” (Allaah Akawaambia): “Msije kusema Siku ya Qiyaamah (kwamba) hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.” Au mkasema: “Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. [Al-A’raaf: 172-173]

Roho hizo ni za wanaadamu wote tokea Nabiy Aadam (‘Alayhis-Salaam) mpaka siku ya Qiyamaah. Kwa maana: wanaadamu wote wanaozaliwa au watakaozaliwa leo au kesho au mwakani na kuendelea mpaka Siku ya Qiyaamah, roho zao zimeshaumbwa.

Dalili ni Hadiyth ifuatayo ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuhusu roho kupulizwa tumboni mwa mama anaposhika mimba inayofikia muda wa miezi minne (siku 120:,

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abu ‘Abdir-Rahmaan ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa

((Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).

Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. WaLLaahi, naapa kwa Yule Ambaye hakuna mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye vitendo vya watu wa Peponi hadi ikawa baina yake na pepo ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu wa Motoni akaingia Motoni.

Na mmoja wenu hufanya vitendo vya watu wa Motoni hadi ikawa baina yake na Moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Chanzo: Alhidaayah

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s