Serikali yaigomea UN pendekezo la kuruhusu ushoga

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akiwa pamoja na Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernard Membe
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akiwa pamoja na Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernard Membe

Dar es Salaam. Tanzania imegoma kuridhia pendekezo linalotaka haki kwa watu wenye uhusiano ya jinsia moja kuingizwa katika sheria za ndani lililotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa chini ya mapendekezo ya pamoja ya dunia.

Pendekezo hilo ni kati ya mapendekezo 153 yaliyotolewa kwa Tanzania na baraza hilo Oktoba 2011. Kati ya hayo Serikali ilikubali mapendekezo 107 na kukubali sehemu fulani tu ya mapendekezo 13.

Kutokana na hilo jumla ya mapendekezo 33 yalikataliwa na Serikali likiwamo la hilo.

Akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani iliyohudhuriwa na mabalozi mbalimbali nchini pamoja na wadau, Mkurugenzi Msaidizi, Masuala ya Haki za Binadamu katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Nkasori Sarakikya alisema, baadhi ya mapendekezo yaliyokataliwa ni yale yanayokinzana na utamaduni wa nchi.

Sarakikya aliongeza kuwa yale 107 yaliyoungwa mkono kwani ni muhimu katika uboreshaji wa haki za binadamu nchini.

Sarakikya alieleza kuwa mapendekezo kama ya kutaka kutoa haki kwa watu wenye uhusiano wa jinsia moja, kuondoa utaratibu wa kulipa mahari na ndoa ya mke zaidi ya mmoja, wasichana kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 pamoja ya kutaka hukumu ya kunyongwa ifutwe hayawezi kuingizwa katika sheria za ndani.

Lakini alibainisha kuwa, pendekezo la kufuta umri wa kuolewa na kuufanya ufikie miaka 18 linafanyiwa kazi kwani kwa namna moja au nyingine linakiuka haki za binadamu.

“Hapo awali tulikataa kwa sababu tusingeweza kufanya uamuzi sisi wenyewe bila kushirikisha viongozi mbalimbali hasa wa dini kwani kuna baadhi ya dini zinaruhusu hilo,” alifafanua.

Hata hivyo, alisema kwenye Katiba Inayopendekezwa suala la umri wa kuolewa limezungumziwa na kwamba mapendekezo yamepitishwa kuwa umri wa kuolewa uongezwe hadi kufikia miaka 18.

Akisoma hotuba yake, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi alitoa rai kwa Serikali kukubaliana na baadhi ya mapendekezo likiwamo lile linalopinga wasichana kuolewa wakiwa na umri mdogo.

“Natumaini kuwa Serikali hii itafikiria na baadaye kuyapitisha mapendekeo hayo. Mfano suala ya wasichana kuolewa wakiwa na umri wa chini ya 14. Hilo ni jambo la msingi ambalo linatakiwa kuzingatiwa kwani linaenda kinyume na haki za binadamu,” alisema Sebregondi.

Mbali na ombi hilo balozi huyo aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi ambazo imekuwa ikifanya za kupambana na mambo mbalimbali yanayohusiana na uvunjivu wa haki za binadamu.

Alisema licha ya juhudi hizo bado kuna changamoto inayohusiana na masuala ya haki za binadamu.

Mapendekezo hayo yaliondolewa na Serikali kwa kuwa, kwa namna moja au nyingine yalionekana kutoendana na mtazamo wa wananchi walio wengi na kwamba sheria zilizopitishwa zinatakiwa kufanyiwa kazi.

Chanzo: Mwananchi

Soma hotuba kamili hapa: – http://www.eeas.europa.eu/delegations/tanzania/documents/press_corner/20141210_01_en.pdf

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s