Polisi wakamata shotgun nyumbani kwa mwekezaji Z’bar

Baadhi ya fukwe za bahari katika visiwa vya Zanzibar ambapo Wawakezaji wengi huwekeza hoteli katika maeneo hayo
Baadhi ya fukwe za bahari Zanzibar ambapo Wawakezaji wengi huwekeza hapo

Zanzibar. Mwekezaji ambaye ni raia wa Ufaransa (jina tunalihifadhi), anasakwa na polisi kwa madai ya kumiliki bunduki aina ya Shotgun iliyokamatwa nyumbani kwake eneo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.

Bunduki hiyo ilikutwa chumbani kwa mwekezaji huyo akiwa ameihifadhi juu ya kabati akiwa ameifunga kwa taulo. Pia Polisi walikamata risasi 10 za silaha hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi alisema Polisi wamefanikiwa kukamata silaha hiyo kutokana na taarifa walizopewa na raia mwema.

Alisema baada ya kufanyika upekuzi kwenye nyumba hiyo, walifanikiwa kuikamata silaha hiyo yenye namba NK 43 EM iliyotengenezwa nchini Urusi na polisi inaendelea kumsaka mwekezaji huyo anayemiliki hoteli moja ya kitalii katika Ukanda wa Pwani ya Paje.

Alisema kwa mujibu wa sheria namba 6 (3) na namba 2 ya mwaka 1991 ya Silaha Tanzania Sura ya 223, mtu yeyote akiwa Zanzibar haruhusiwi kubeba, kumiliki au kutumia silaha au risasi isipokuwa kwa kibali maalumu.

Aidha, alisema mbali na silaha hiyo, polisi pia walikamata mkebe maalumu wa kuhifadhia bastola ambayo ilikamatwa katika tukio la kujeruhi lililotokea nyumbani kwa mwekezaji huyo Novemba 23, mwaka huu.

Alidai kuwa hii ni mara ya pili kwa mwekezaji huyo kutuhumiwa kumiliki silaha kinyume na sheria na tayari anadaiwa kujeruhi watu sita wakiwamo waandishi wa habari wawili. Katika tukio la kwanza, alifikishwa mahakamani na aliachiwa kwa dhamana.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s