Hatima ya ugaidi kesi ya Uamsho wiki ijayo

UamshoDar es Salaam. Jaji Fauz Twaib wa Mahakama Kuu wiki ijayo atatoa uamuzi wa maombi ya kufutiwa mashtaka ya ugaidi yanayowakabili viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki).

Mawakili wa washtakiwa hao walifungua maombi hayo Oktoba 13, 2014, wakitaka Mahakama Kuu ifanye marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu ya kukataa kusikiliza ombi hilo kwa kuwa haina mamlaka hayo.

Hata hivyo, upande wa mashtaka uliweka pingamizi la awali dhidi ya maombi hayo, ukiomba yatupiliwe mbali kwa madai kuwa hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo, ina dosari za kisheria na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza maombi hayo.

Pingamizi hilo la Jamhuri lilisikilizwa jana na Jaji Dk Fauz Twaib ambaye baada ya kusikiliza hoja za pande zote, alipanga kutoa uamuzi huo Jumatano ijayo, Desemba 10, 2014.

Ikiwa Jaji Twaib atakubaliana na hoja za pingamizi hilo la Serikali, maombi hayo yatatupiliwa mbali na hivyo washtakiwa hao kuendelea na mashtaka hayo au watalazimika kuchukua hatua nyingine kadri mahakama itakavyoelekeza katika uamuzi wake.

Haa hivyo, kama mahakama itatupilia mbali hoja za pingamizi hilo, kesi hiyo itandelea na usikilizwaji wa maombi ya msingi na hatimaye kutoa uamuzi wa kuyakubali au kuyakataa.

Katika maombi yao yaliyofunguliwa chini ya hati ya dharura, washtakiwa wanaiomba Mahakama Kuu iitishe na kuchunguza kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo, ili kujiridhisha na uhalali na usahihi wake.

Pia wanaiomba mahakama hiyo itupilie mbali hati ya mashtaka waliyofunguliwa Septemba 3, mwaka huu, wakidai kuwa imefunguliwa bila ya ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka.

Washtakiwa hao pia wanaiomba mahakama hiyo itupilie mbali hati ya mashtaka kwa kushindwa kuweka wazi maelezo ya makosa ya ugaidi yanayodaiwa kutendwa na Sadick na Furaha.

Pia wanaiomba mahakama hiyo itupilie mbali hati ya mashtaka kwa kushindwa kuonyesha wazi majina ya watu ambao waliandaliwa kwa ajili ya kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Katika mbadala wa maombi hayo ya juu, pia washtakiwa hao wanaiomba mahakama hiyo iamuru kuwa kila mshtakiwa ashtakiwe mahakama yenye mamlaka katika maeneo walikokamatiwa.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s