Mahakama yamtakasa Sheikh Issa Ponda

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda
   Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemtakasa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai iliyotokana na mgogoro wa ardhi wa Chang’ombe Markazi.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Agustine Shangwa baada ya kuridhika na hoja za rufani za Sheikh Ponda kupitia kwa Wakili wake, Juma Nassoro kupinga hukumu na hatia ya Mahakama ya Kisutu.

Mbali na kumfutia hatia hiyo, pia Jaji Shangwa alimshauri Sheikh Ponda kufungua kesi ya madai dhidi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), pamoja na Kampuni ya Agritanza Ltd iliyonunua eneo la Chang’ombe Markazi.

Ponda alikata rufani mahakamani hapo akipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai namba 245 ya mwaka 2012, iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake 49.

Katika rufaa hiyo, Sheikh Ponda kupitia kwa wakili wake, Nassoro aliwasilisha jumla ya hoja sita za kupinga hukumu hiyo.

Hoja hizo zilikuwa ni pamoja na ya kudai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kumtia hatiani kwa kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa kosa hilo la kuingia kwa nguvu katika eneo hilo la mgogoro.

Pia alidai kuwa mahakama ilikosea kumtia hatiani na kuwaachia huru washtakiwa wenzake.

, kwa kutumia ushahidhi huohuo, na kwamba kesi hiyo ilikuwa ikihusu mgogoro wa ardhi hivyo Polisi walipaswa kumshauri mlalamikaji akafungue kesi ya madai katika Mahakama ya Ardhi.

Hata hivyo katika hukumu yake Jaji Shangwa alijikita katika hoja moja tu kama kulikuwa na ushahidi wa kutosho kumtia hatiani mrufani.

Akijibu hoja hiyo katika hukumu yake, Jaji Shangwa alikubaliana na Wakili wa mrufani kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mrufani bila kuacha mashaka.

Jaji Shangwa alisema kuwa hakuna ushahidi kuwa mrufani aliwashinda mkono au kuwahamaisha wale watu aliokuwa akishitakiwa nao kwenda katika eneo hilo, bali wale watu walikwenda pale wenyewe baada ya kutangaziwa katika misikiti yao kuwa kuna ujenzi wa msikiti wa muda katika eneo hilo.

“Kama hakufanya hivyo utasema kuwa aliingia kwa nguvu? Nakubaliana na hoza za wakili wa mrufani, Nassoro kuwa hakuna ushahidi wa kutosha mahakama kumtia hatiani mrufani bila kuacha mashaka.”, alisema Jaji Shangwa.

 Chanzo: Mwananchi

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s