CCM isiwafumbie macho wazanzibari wanaosaka urais kinyume na taratibu

Baadhi ya wanachama wa Cahama Cha Mapinduzi wameanza kampeni za chini kwa chini hapa Zanzibar wakisaka urais
Wapo baadhi ya wanachama wa Cahama Cha Mapinduzi wameanza kampeni za chini kwa chini hapa Zanzibar wakisaka urais

Na Abdallah Vuai, Zanzibar

Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia neno ‘propaganda’ kama nadharia isiyokuwa sahihi, yenye kufikirika na iliyosheheni chembe ya shaka,lakini neno hilo maana yake ni aina fulani ya mawasiliano yenye kushawishi jamii kuunga mkono suala jambo linalokusudiwa ambapo yale yaliyolengwa ni ya upande mmoja tu.

Kwa hivyo, propaganda ni uenezi wa nadharia fulani katika jamii. Na kwa kawaida inakuwa na sura mbili moja ni uhalisi na pili kupotosha itikadi inayopingana na hiyo unayoeneza.

Wanasiasa wamekuwa wakilitumia sana neno hilo ambalo linawasaidia kuenez itikadi zao kwa uhalisi wake ili kuwavuta watu waipende na pia kupotosha itikadi pinzani ili ichukiwe.

Tumeona,tumesikia, baadhi ya wanasiasa  hapa Zanzibar wakieneza kampeni za kutaka kuchukuwa fomu ya kuwania urais kupitia CCM kinyume na utamaduni, mazoea na mila za Chama hicho.

Wanasiasa hao wanatumia  propaganda ‘dhaifu’ kujenga uhalali wa wao kutaka kuchukuwa fomu huku wakiwa hawana hoja zenye kueleweka.

Kwa kawaida propaganda yoyote ya kupotosha hufa pale tu muda unapokwisha na lengo lake kutimia. 

Kama itikadi yako inapotoshwa basi utajikuta unashughulishwa usiende mbele ubakie katika mtego wa buibui huku ukipoteza muda na nguvu  kujibu mapigo na kumwacha mpinzani wako akiwa likizo na aweze kupanga mipango ya kwenda mbele.

Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameling’amua hilo na ndio maana hawakuweza kuingia kwenye mtego wa Buibui na nbadala yake aliwapuuza wale wanaopita pita na propaganda kama ile ya popobawa.

Ama kweli kikulacho kinguoni mwako, rafiki yako mwema  wa leo kesho anaweza kugeuka akawa adui yako hatari na adui si ajabu ukamkuta akiwa mshirika  mtiifu ,pika pakua,nyakati za msiba na sherehe masika au kiangazi.

Lakini nafikiri huo ndiyo mchezo wa siasa ambao unaelezwa kukosa fomula halisi wala kanuni za kuendesha mchezo huo ambao umegharimu mamimlioni ya maisha ya watu,kuwapa faraja,hadhi na utukufu huku wengine wakiishi magerezani

Katika siku za hivi karibuni, hapa Zanzibar kumeibuka  harakati , baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi wakifanya kampeni za kuwania Urais kwa tiketi ya Chama hicho kinyume na mila au utamaduni wa CCM mwaka 2015.

Tayari kuna vikundi kazi  vya kisiasa vimeundwa ,miongoni mwa watu wanaotajwa kuwa na nia ya kutaka kuchukua fomu kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM ni vigogo wa juu wa chama hicho.

Wanasiasa wameanza kampeni  za mbio za urais mwaka 2015 , sasa wakitaka kumpiku na kumpoka tiketi Rais aliyepo madarakani Dk Ali Mohammed Shein ,wakipitapita  ,kuchafua hali ya hewa na kuanza kumnadi mtu wao kinyume na taratibu za CCM. 

Inashangaza kuona CCM ikiwachukulia hatua baadhi ya wanachama wake kwa upande wa Tanzania Bara wanaofanya kampeni mapema,lakini ikifumbia macho wapigadebe na wanachama wake kwa upande wa Zanzibar

Wiki ilopita alionekana mjumbe mmoja wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM akiendesha kampeni za kumpigia debe mmoja kati ya wagombea wanaotajwa kutaka  nafasi ya urasi bila soni wala kimeme kinyume na utaratibu wa Chama chake.

Mjumbe huyo wa NEC akakutana na Naibu Waziri mmoja wa Zanzibar akimshawishi amuunge mkono mgombea wao katika pirika za kuwania Urais, ingawa haikueleweka kama kigogo huyo alikubali au la.

Wadadisi wa mambo ya siasa Visiwani humu  wanasema kumekuwa na vikao kadhaa vinavyofanyika baina ya Zanzibar na Dar es Salaam vya kupanga mikakati ya  namna gani wanavyoweza kumnadi mwanasiasa wao mbele ya wapigakura wa CCM na katika vikao vya maamuzi vya Chama hicho.

Ingawa hadi sasa hakuna mwanasiasa yeyote aliyesimama hadharani na kusema atagombea nafasi hiyo  kwa kuvunja mwiko na mila za CCM, wapambe wamekua wakipita pita sehemu mbalimbali kumnadi na wakitumia mbinu za kudai eti CCM  Zanzibar imedorora!

Ikumbukwe wanaofanya kampeni hizo ni kundi la  itikadi ya kihafidhina hapa Zanzibar  na licha ya kupewa madaraka wameshindwa kuonyesha uwezo,umakini na uthabiti wa kuwa viongozi wa juu.

Mtu mwenye busara anaweza kujiuliza watu au mtu huyo ana jipya gani ambalo anataka kuwafanyia wananchi wa Zanzibar ilihali alipata fursa ya kuwa viongozi  wa juu na kujikuta wakishindwa katika usimamizi?

Dk Sheina anatajwa kuwa ndiye kiongozi mwenye siasa za wastani,makini na hodari wa kupima mivumo ya pepo za kisiasa na kuwavumilia wapinzani wake hata pale wanapoteleza na kumpiga vijembe vya hadharani.

Chanzo: Mwananchi

One Reply to “CCM isiwafumbie macho wazanzibari wanaosaka urais kinyume na taratibu”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s