Urais si mashindano ya urembo – Maghembe

Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti hili, walipomfanyia mahojiano maalumu ofisini kwake mjini Dodoma, hivi karibuni. Picha na Emmanuel Herman
Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti hili, walipomfanyia mahojiano maalumu ofisini kwake mjini Dodoma, hivi karibuni. Picha na Emmanuel Herman

Dodoma. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe ameshangazwa na utitiri wa watu wanaotaka kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, akisema nafasi hiyo ya juu nchini haifanani na mashindano ya urembo ambayo mtu yeyote anaweza kujaribu.

Mbunge huyo wa Mwanga alisema watu hao wanaojitokeza kuwania urais hawaelezi wanataka kulifanyia nini Taifa na akashauri wasioweza kueleza hoja zao wasichaguliwe kushika nafasi hiyo.

“Urais unahitaji kuwa na sifa, dira na ajenda kwa Taifa,” alisema Profesa Maghembe wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa.

Kauli ya Profesa Maghembe imekuja wakati Taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2015, huku chama chake, CCM kikikabiliwa na kazi ngumu ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake.

Hali kama hiyo iliikumba CCM wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 wakati takriban watu 20 walipojitokeza kutaka kuingia Ikulu na baadaye mwaka 2005 wakati wa uchaguzi uliomuweka madarakani Rais Kikwete.

Ndani ya CCM, mjadala huo sasa umekumbwa na hoja ya umri baada ya makada vijana kujitokeza kutangaza nia ya kumrithi Rais Kikwete kupambana na wanasiasa wakongwe, baadhi wakiwa ni wale waliojiandaa kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Profesa Maghembe alipuuza mjadala huo wa umri wa mtu kugombea urais akisema kuwa hauna msingi na kwamba sifa kuu ya mgombea urais ni ajenda ya kuliletea Taifa maendeleo endelevu.

“Umri hauwezi kuleta tofauti katika uongozi wa nchi. Ni kama kusema jiwe liwe rais,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye amefanya kazi wizara tofauti tangu Januari 2006 aliposhika uwaziri kwa mara ya kwanza.

Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka mgombea urais awe na umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea.

“Hivyo haisemi kuwa ukishakuwa na miaka 70 huwezi kuwa rais ama haisemi ukiwa na miaka 40 unafaa zaidi kuwa rais. Inategemea huyo mtu anayegombea anataka kuwafanyia nini Watanzania,” alisema.

Waziri huyo wa saba tangu Wizara ya Maji ianzishwe, alisema kugombea urais kunategemea ajenda aliyonayo mtu na hata watu wanapokwenda kumchagua, lazima waangalie ana ajenda gani. “Ikulu si mahali pa kukimbilia, mimi hata sijui wanakimbilia nini kwa sababu lazima mtu uwe na ajenda. Na kama mnasikia mtu anasema mimi nataka kuwa tu rais, huyo hafai kabisa,” alisema.

“Lazima mtu anayetaka kuwa rais atueleze uchumi sasa unakua kwa asilimia saba na umekuwa hivi kwa karibu miaka 10 lakini ni jambo linalofanya umaskini uwe mkali kabisa na usiishe ni kutokana na shughuli inayofanywa na watu wengi ya kilimo, kuwapatia kipato haikui kama sekta nyingine.

 

Advertisements

One Reply to “Urais si mashindano ya urembo – Maghembe”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s