Serikali ya Umoja wa Kitaifa yairejesha ZNZ katika ustaarabu

Katikati ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein akiwa na Kamati ya watu sita ya kusimamia Maridhiano
Katikati ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein akiwa na Kamati ya watu sita ya kusimamia Maridhiano.

Ujio wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na mageuzi ya hali ya siasa ni moja kati ya mambo ambayo leo yameifanya Zanzibar na watu wake kuwapo katika ramani ya mwelekeo wa kilele cha demokrasia si tu Afrika, bali kuzishinda hata nchi za Ulaya ambazo baadhi yake demokrasia inasuasua.

Ingawa haikuwa jambo jepesi kubadili mambo yaliyokuwa yamezoeleka kwa miaka mingi, hatimaye viongozi waliweka kando utashi binafsi na kutanguliza maslahi ya wengi katika ujenzi wa jamii mpya Zanzibar.

Matakwa ya kisiasa yaliyobadilisha mfumo wa Serikali Zanzibar kuwa ya Umoja wa Kitaifa ni sehemu ya mtangamano wa siasa za kistaarabu, kiungwana hivyo, katika kipindi hiki tusingesikia tena matamshi ya kutaka kurudi nyuma au kuyumbisha maridhiano ya kisiasa.

Matamshi yanayotolewa na wapinga SUK yanatia kichefuchefu, yanakirihisha. Ni muhimu kwa wanasiasa kuchunga matamshi yao.

Lakini hata wale wahafidhina waliokuwa hawataki maridhiano yaliyozaa SUK wanawajibika kuweka mkazo katika maslahi ya wengi.

Bila amani, utulivu, umoja na uzalendo, hakuna maendeleo. Hata kama utakuwa na rasilimali za aina kwa aina, yakikosekana mambo hayo hakuna liwalo zaidi ya vurugu na uporaji wa rasilimali za nchi kama tunavyoshuhudia katika baadhi ya Nchi.

Ni jambo la kawaida kuona kwamba tabia ya mabadiliko katika Siasa si suala lenye kuchanganya watu, au kuparaganya jamii kwani dunia imekuwa ikipitia vipindi mbalimbali vya mabadiliko ambayo kila yatokeapo mara nyingine huamsha hisia tofauti katika maisha ya raia.

Hali kadhalika, madaliko kama vile ya kimsimu, mvua na jua, theluji, masika na kiangazi, yanaendelea kila mwaka na kufikia hali ya kuzoeleka kiasi kwamba yanapokosekana kila kiumbe juu ya uso wa nchi huingia wasiwasi, huzuni na shaka si tu kuelekea mabadiliko husika bali hasa katika kuhofia maisha yake ya kesho.

Umuhimu wa amani na utulivu, umoja na mshikamano ni mkubwa zaidi kuliko jambo lolote lile kwani ghasia zinazosababisha umwagikaji wa damu katika nchi zisizotulia kisiasa, zilianza kama cheche.

Pengine tunatupia jicho tu sehemu zile ambazo risasi na mabomu yanarindima kila sekunde, lakini hatuna budi kuangalia hapa petu. Wanasiasa na wananchi wa kawaida wanaotoa matamshi ya kuchochea vurugu, tunawafanyeje?

Kiongozi makini na mwenye kujali wale anaowaongoza ni lazima awe mfano wa uwajibikaji, uadilifu na uzalendo. Baadhi ya wanasiasa wanataka kuturejesha katika siasa za chuki, uhasama na ubaguzi. Hawa wanajifanya kutumia hoja mbalimbali kufanikisha yao. Lakini wahenga wetu wanatuasa kwamba mtu mwenye fikra njema katika jamii huacha fahari au sifa kwa vizazi vya nyuma, lakini ni tafakuri ya fahamu ya jambo maana kama ingelikuwa akili ni maneno, hakuna atakayemshinda kasuku.

Watu wenye busara mara nyingi wanawatendea mazuri raia wenzao katika nchi na kwa hakika maisha yanaisha kwa mtu huyo kukumbukwa na jamii kwa wema wake,,lakini wapo pia ambao hukumbukwa kwa maovu na ubaya wao.

 Chanzo: Mwananchi

 

 

Advertisements

One Reply to “Serikali ya Umoja wa Kitaifa yairejesha ZNZ katika ustaarabu”

  1. “Wanasiasa na wananchi wa kawaida wanaotoa matamshi ya kuchochea vurugu, tunawafanyeje?
    Hawa tumwachie Mungu awashugulikie. Najua wanaomba hali irudie kama nyuma wawapeleke jamaa zao sehemu za machufuko wakirudi wawaletee ngawira za mapambo na vitu vya matumizi ya nyumbani

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s