Jaji Mutungi:Ruzuku ni changamoto kwa Ukawa

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unakabiliwa na changamoto kubwa suala la ruzuku. Ingawa hakutaka kuingia kwa undani kuelezea changamoto hiyo, Jaji Mutungi alisema anaona ugumu wa Ukawa katika kushughulikia tatizo hilo, lakini akaongeza kuwa wakati ukifika ofisi yake italizungumza.

Alisema hayo jana alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu uamuzi wa vyama hivyo vinne kuamua kushirikiana katika chaguzi zijazo na tafsiri yake kisheria.

Jumapili Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF vilisaini makubaliano ya kushirikiana katika mambo saba, likiwamo la kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote kuanzia chaguzi za serikali za mitaa hadi Uchaguzi Mkuu ujao.

Jaji Mutungi alisema: “Maswali hayo unapaswa kuwauliza wao. Tutakuja kuzungumza wakati ukifika. Suala la ruzuku lina taratibu zake, Muungano una taratibu zake na ushirikiano pia,” alisema.

“Ruzuku ni changamoto katika suala la Ukawa, lakini sitaki kuingilia hilo kwa kuwa ukifika wakati tutasema.”

Alisema kwa sasa nchi inaelekea katika uchaguzi, hivyo ni muhimu kwa Ofisi ya Msajili ikaacha kuingilia hayo. “Lazima niwe careful (makini) katika mazungumzo yangu, kwani naweza nikawa mimi na wewe (mwandishi) tunatafsiri sheria, lakini wengine wakafikiria kisiasa,” alisema Jaji Mutungi.

Kifungu cha 18 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2002 kinaeleza kuwa ruzuku ambazo chama kitapewa zitakuwa ni kwa ajili ya shughuli za chama husika bungeni, shughuli za kijamii za chama husika, suala lolote la uchaguzi ambalo chama kimeteua mgombea na kitu chochote muhimu ambacho chama kitakuwa kinafanya.

Kifungu hicho kinaeleza kuwa ruzuku ambazo chama kinapata lazima zikaguliwe na kuwasilishwa hesabu kwa Msajili wa Vyama.

Changamoto hiyo inatokana na ukweli kwamba kuunganisha nguvu kutamaanisha kuwa chama kitakubaliwa na Ukawa kusimamisha mgombea urais, ndicho kitakachonufaika na ruzuku, ambayo kwa kiasi kikubwa hutokana na uwingi wa kura anazopata mgombea wa nafasi hiyo.

Chadema, ambayo mgombea wake wa urais katika uchaguzi uliopita, Dk Wilbroard Slaa alipata kura 2,271,941, kinapata ruzuku ya Sh203.6 milioni kwa mwezi, wakati CUF inapata ruzuku ya Sh117.4 milioni baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kupata kura 695,667.

NCCR-Mageuzi inapata ruzuku ya Sh10 milioni wakati NLD haipati ruzuku yoyote kutokana na kutokuwa na wabunge.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s