Moyo afafanua kilichotokea uchaguzi wa 2010

Wagombea wa kiti cha urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2010 Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) na Dk Ali Mohammed Shein (CCM) wakipeana mkono wa furaha baada ya kutolewa kwa matokeo hayo hapo ukumbi wa Salama Bwawani ambapo sio lolote zaidi ya "Spirit" ya Maridhiano tu ndio iliyotawala kwa wakati ule.
Wagombea wa kiti cha urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2010 Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) na Dk Ali Mohammed Shein (CCM) wakipeana mkono wa furaha baada ya kutolewa kwa matokeo hayo hapo ukumbi wa Salama Bwawani ambapo sio lolote zaidi ya “Spirit” ya Maridhiano tu ndio iliyotawala kwa wakati ule.

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Hassan Nassor Moyo, anaamini ushawishi wake kwa kiongozi wa CUF, Seif Sharif Hamad, ulichangia kuinusuru Zanzibar isitumbukie kwenye umwagikaji damu mwaka 2010.

Kufuatia taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Tanzania juu ya nafasi ya Mzee Moyo kwenye uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2010, Josephat Charo alizungumza na mwanasiasa huyo ambaye alikuwa mjumbe kwenye Baraza la kwanza la Mapinduzi la Zanzibar chini ya Marehemu Abeid Karume, Waziri wa Sheria wa Muungano, Waziri wa Elimu wa Zanzibar na sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano, juu ya mchango wake huo, hasa kwa kuwa vyombo vya habari viliandika chama tawala cha CCM kilikuwa tayari kwa lolote lakini sio kutangazwa mgombea wa kilichokuwa chama cha upinzani, CUF, kama mshindi wa urais kwenye uchaguzi huo.

Katika mahojiano haya, Mzee Moyo kwanza anaelezea vipi aliweza kumshawishi mgombea wa CUF, Seif Sharif Hamad, akubali ushindi wa mpinzani wake mgombea wa CCM na rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza hapa 

Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 

 

One Reply to “Moyo afafanua kilichotokea uchaguzi wa 2010”

  1. Kwa kweli maalim serif in kiongozi mwadilifu mkweli muungwana mzanzibar halisi si was kuchovya anayejali wananchi wake.nashangazwa name ubaguzi wa upemba dharau za kijinga hats kwa rais wao wapemba wako juu chuki zenu bure.kura ya maoni hapa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s