Kesi ya padri Mushi mtegoni

Padri wa Kanisa Katoliki, Evaristus Mushi aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiegesha gari kando na Kanisa la Mtoni.

Padri wa Kanisa Katoliki, Evaristus Mushi aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiegesha gari kando na Kanisa la Mtoni.

OKTOBA 3 mwaka huu inaweza kuwa siku ya mwisho kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wa Zanzibar kutoa kisingizio cha kutokamilika kwa upelelezi wa kesi ya mauaji ya Padre Evarist Mushi kwani jaji anayeisikiliza amesema hawezi kuridhia kisingizio hicho.

Jaji Omar Othman Makungu amesema kesi hiyo kwa namna mwenendo wake ulivyo, haistahili tena kuwepo mahakamani. Anahofia kuwa inaweza kuendelea hivyo hata upande wa mashitaka ukipewa miaka miwili mingine. Continue reading

Wataka posho ya Sh500,000 kwa siku

Baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba

Baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba

Dodoma. Mzimu wa posho umeibuka upya katika Bunge la Katiba, safari hii wajumbe wake wa Kamati ya Uandishi wakiomba walipwe posho maalumu ya Sh500,000 kwa siku kutokana na kazi ya kuandika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge zinasema kuwa tayari maoni ya wajumbe yamewasilishwa kwa uongozi kwa ajili ya uamuzi. Continue reading